Wednesday, February 25, 2015



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameibua tuhuma nzito dhidi ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akisema kuwa wamekaidi ushauri wa kitaalam uliowazuia wasitumie mfumo mpya wa Biometric Voter Registration (BVR) katika uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Mbowe amedai kuwa baada ya kuona zoezi la kuandikisha wapiga kura haliendi kama ilivyotakiwa, NEC walimtafuta mshauri mwelekezi aitwae Darrell Geusz, mtaalam wa masuala ya BVR kutoka Marekani ambaye baada ya kufanyia utafiti ‘hali’ ya Tanzania kuhusu mfumo huo mpya, aliwaambia wakilazimisha wanaweza kusababisha machafuko ya kisiasa nchini.

Kwa mujibu wa Mbowe, mtaalam huyo katika ripoti yake aliyoitoa mwezi Januari mwaka huu, aliiambia NEC kuwa kwa sasa Tanzania haiwezi kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa BVR kwa sababu ya ukosefu wa fedha, vifaa, utaalam na muda kwani mfumo huo ili uweze kufanya kazi inayotakiwa unahitaji maandalizi ya takriban mwaka mmoja.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ameyasema hayo jijini Mbeya wakati alipohutubia matukio mawili tofauti, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika mikoa ya Kanda (ya CHADEMA) ya Nyanda za Juu Kusini yenye mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma na Rukwa.

Mapema asubuhi Mwenyekiti Mbowe alihutubia wakati akifungua kikao cha Baraza la Uongozi wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kisha baadae jioni akahutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Dk. Slaa mjini Mbeya.

“Mshauri huyo mwelekezi ambaye ni mtaalam wa masuala ya BVR kutoka Marekani, amewahi kuisaidia nchi ya Bangladesh ambako waliandikisha wapiga kura milioni 80, aliwaambia NEC kuwa Tanzania hatuwezi kuendesha hili zoezi kwa sasa, hatuna vifaa, hatuna wataalam, hakuna muda wa kutosha, hatuna wataalam, hatuna maandalizi, akawatahadharisha wakilazimisha wanaweza kusababisha machafuko.

“Lakini katika hali ambayo haijulikani, wakiendeleza ukaidi kwa ajili ya kutaka kuibeba CCM, NEC inaonekana kutaka kuendesha zoezi hili bila kuzingatia ushauri wowote wa kitaalam wala kushirikisha wadau ambao ni vyama vya siasa wala haitaki kutoa taarifa za kutosha kwa wananchi ambao ndiyo wapiga kura wenyewe.

“NEC imekuwa ikiendesha suala hili kwa usiri usiri sana, taarifa zao wanapoamua kutoa zimekuwa za kusua sua sana, kwa kushtukiza. Tumekuwa tukidai ushirikishwaji wa kina wa shughuli na mfumo huu bila mafanikio. Tumeomba sana kupata nyaraka ili tuelewe, lakini hawataki. Wanafanya siri kubwa.

“Sasa nasi kwa sababu tunazo njia mbalimbali za kupata taarifa, tumezipata nyaraka ambazo hawataki wadau kwa maana ya vyama vya siasa tuzione.

Kwanza tumepata nyaraka ambayo inaonesha kuwa wakati walikuwa wanasema hawana kitu cha kutupatia ili tuelewe mfumo huu wa BVR, wao labda na CCM yao tangu 2013 walikuwa tayari wanajua kitakachofanyika.

“Lakini pia tumefanikiwa kupata nyaraka nyingine hii hapa. Hawa jamaa wa NEC baada ya kuzidiwa wakaamua kutafuta mshauri mtaalam kutoka Marekani ambaye anasifika duniani, yaani katika masuala ya BVR ni authority, ameandika ripoti yake yenye kurasa 16, amewapatia hadi ushauri wa tahadhari ya madhara ya kiusalama jamaa wa NEC na Serikali ya CCM hawataki kusikia,” amesema Mbowe.

Mbowe ameongeza kusema kuwa wakati mshauri huyo mtaalam wa BVR akiwatahadharisha NEC kuhusu muda, tume imeendelea kusema kuwa zoezi hilo litafanyika na kufanikiwa kwa kipindi cha ndani ya miezi miwili, jambo ambalo Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kuwa serikali inacheza na ‘roho ya amani katika nchi’.

Alisema kuwa mazingira yanayoendelea nchini Tanzania katika suala la mchakato wa hatua mbalimbali za uchaguzi mkuu wa mwaka huu, yanatengeneza hali ya kutokuaminiana miongoni mwa wadau, akisema kuwa hali hii husababisha uchakachuaji na katika nchi zingine imesababisha machafuko ya kisiasa.

NEC na ubabaishaji katika ratiba

Mbowe amesema kuwa tangu mwaka jana NEC imekuwa ikitoa taarifa za kukanganya kuhusu ratiba kamili ya kuanza kuandikisha upya wapiga kura nchi nzima, ambapo iliwahi kusema shughuli hiyo ingeanza Septemba 2014, baadae ikaahirisha hadi Desemba, lakini pia haukufanyika, kisha baadae ikatoa ratiba ya kuanza kazi hiyo Februari 16 mwaka huu, ikianza na mikoa minne ya Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

Kiongozi huyo amesema kuwa baada ya vyama vya siasa kuibana NEC juu ya ratiba na maandalizi muhimu kuhusu shughuli hiyo huku muda ukikaribia, tume ikawaita wadau na kuwaambia kuwa zoezi limesogezwa mbele ili kuvipatia vyama vya siasa muda wa kuandaa mawakala, hivyo litaanza Februari 23, mkoa mmoja pekee wa Njombe badala ya mikoa minne kama ilivyotangazwa awali.

“Tukawaambia mnasema tuwaandae mawakala wetu, tuwaandae kuhusu kufanya majukumu yapi hasa na hamtaki kutupatia nyaraka, bado wakaendelea kutoelewa. Tukawaomba hata ratiba ya mkoa huo mmoja bado hawakuweza kutupatia. Yaani ni ubabaishaji tu. Sisi tukaamua kupeleka watu wetu huko mkoa mzima kuanza maandalizi. Tayari tunavyozungumza tuna watu wako field.

“Katika hali ya kushangaza sana, jana tukapokea ratiba yao, wakaongeza maajabu mengine tena. Ratiba yao inaonesha kuwa hata mkoa mmoja wa Njombe pekee wameshindwa kuandikisha mkoa mzima badala yake wataanza na jimbo moja tu la Njombe Kaskazini. Katika jimbo hilo pia hawawezi kuandikisha kata zote kwa wakati mmoja badala yake wataanza na kata mji mdogo wa Makambako.

“Yaani wameshindwa mikoa minne, wakaamua mkoa mmoja, mkoa mmoja hawawezi kuandikisha wilaya zote, hata wilaya moja wameshindwa, wataanza na jimbo moja na katika jimbo hilo wataandikisha kata 12, sio zote kwa pamoja wataanza na kata 9 za mji mdogo wa Makambako, kisha zitafuata kata zingine. Hii ni aibu ya hatari,” amesema Mbowe na kuongeza;

“Yaani wakati mamilioni ya Watanzania wanasubiri kuandikishwa nchi nzima, NEC haiwezi hata kuandikisha wilaya moja kwa wakati mmoja. Halafu eti wameniandikia barua ya mwaliko kwenda Makambako kushiriki hafla ya uzinduzi utakaofanywa na Waziri Mkuu Pinda siku ya Jumanne ijayo, nawauliza viongozi wenzangu niende nisiende.

“Kwa sababu kwenda kwenye uzinduzi huo wa NEC utakaofanywa na Waziri Mkuu ni kubariki uhuni wote huu wanaoufanya.”

Serikali kufilisika, ukosefu wa vifaa vya BVR na kuchezea Sheria

Mwenyekiti Mbowe ameshusha tuhuma nzito kwa Serikali ya CCM akisema kuwa kushindwa kupatikana kwa vifaa vya BVR kwa muda unaotakiwa ili wananchi waanze kuandikishwa kunatokana na serikali hiyo kufilisika, kukosa vipaumbele, kuendekeza ufisadi na matumizi ya anasa huku pia ikilifanya zoezi la uchaguzi kuwa ni tukio la dharura badala ya mchakato wenye maelekezo ya kikatiba.

Alisema kuwa kugeuza uchaguzi kuwa tukio la dharura badala ya takwa la kidemokrasia lenye masharti ya kisheria ni kucheza na haki na matumaini ya Watanzania jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani ya nchi.

“Ili kuandikisha wapiga kura nchi nzima, NEC ilihitaji vifaa…wanaviita BVR kits vipatavyo 15,000 lakini Serikali ya CCM ikawaambia hapana wapunguze, wakapunguza hadi 8,000, katika hivyo 8,000 hadi sasa vipo 250 pekee tangu wakati wa uandikishaji wa majaribio. Hadi sasa vingine havijafika kwa sababu serikali haijalipia, haijalipa kwa sababu imefilisika.

“Pamoja na mazonge haya yote, juzi nimemsikia Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lubuva akisema daftari hili hili watakaloandikisha litatumika kwenye Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, huyu mzee tunamheshimu sana lakini wamempatia kazi itakayoondoa heshima yake. Huyu ni mwanasheria, Jaji mstaafu. Sitaki kuamini kuwa hajui kuwa kuhakiki daftari kabla halijaanza kutumika ni hitaji la kisheria.

“Sheria inaagiza kwamba baada ya uandikishaji lazima wapiga kura wahakiki daftari lao kisha sasa ndipo tunapata daftari la kudumu la wapiga kura. Sasa kwa ratiba yao wanamaliza kuandikisha Aprili 29 na kesho yake Aprili 30 kura ya maoni inapaswa kupigwa, sasa sijui anataka kutumabia nini.

“Pamoja na kwamba sisi kama CHADEMA pamoja na wanachama wenzetu wa UKAWA tumewaomba Watanzania kutoshiriki kupiga kura ya maoni ya katiba ili wasitumike kuhalalisha mchakato haramu, lakini hatutakubali sheria ziendelee kuvunjwa tu waziwazi na akina Lubuva kwa sababu ya maelekezo ya ikulu huku NEC ikitumika tu kama kanyaboya,” alisema Mbowe.

Aliongeza kuwa serikali nyingi duniani hukaribisha machafuko na anguko lake kila zinapoanza kuchezea chaguzi mbalimbali. Alisema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulijulikana miaka 5 iliyopita kikatiba hivyo maandalizi yake hayawezi kuwa ya zimamoto au dharura.

Alisema sheria ya uchaguzi inaelekeza wazi kuwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linapaswa kuboreshwa mara mbili katikati ya uchaguzi mmoja hadi mwingine, lakini hata takwa hilo la kisheria pia limevunjwa na NEC ambayo imeshindwa kuboresha tangu ilipoandikisha mwaka 2010.


Alisema kuwa serikali inayojua wajibu wake kwa wananchi, ilipaswa kujua vipaumbele vya mwaka huu, ikitambua kuwa kuweka mambo makubwa matatu ndani ya mwaka mmoja, yaani; uandikishaji wapiga kura, kura ya maoni ya katiba mpya na uchaguzi mkuu, ni mambo ambayo haiwezi kumudu kuyatekeleza ndani ya muda mfupi, bila kuwa na fedha.

“Yaani wakati Watanzania wenye sifa wakisubiri nchi nzima, taifa zima linasubiri, katika sintofahamu hii, bado viongozi wetu wanathubutu kudanganya kuwa kura ya maoni itafanyika, huku Waziri Mkuu Pinda akienda kubariki mchezo huu keshokutwa huko Makambako. Hatujui wanapata wapi ujasiri huu wa kuwadanganya Watanzania,”amesema Mbowe.

Chanzo chadema blog

BIOMETRIC VOTER REGISTRATION SYSTEM (BVR)



Kumekuwa na sintofahamu kubwa kati ya Tume ya Uchaguzi na Vyama vya Siasa kuhusu kuwasajili watu  kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Kujifunza na kujua ukweli kuhusu uwezekano wa kuwasajili raia wa Tanzania kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya kushiriki kwenye Kura ya Maoni ya Katiba na Uchaguzi Mkuu Ujao wa Mwezi Oktoba tunaweza kujifunza kutoka kwa wenzetu Ghana ambao walifanikiwa kuwasajili Raia wao kwa kutumia mfumo huu wa Computer. 

Baadhi ya Mambo muhimu ya kuzingatiwa katika kufanikisha kusajili watu katika mfumo huu wa Computer ni :-

1. Vifaa yaani seti nzima ya Computer na vifaa vya Fingerprint.

2. Elimu ya kutumia Computer kwa Maofisa wanaoshiriki kwenye zoezi la kusajili


3. Uwepo wa Nishati ya Umeme kwenye eneo husika kwa kuzingatia kwamba vifaa hivi vinatumia Nishati ya Umeme. kwa Vijijini kunaweza kutumia Umeme wa Solar mahali ambapo hakuna nishati ya umeme wa kawaida.


4. Uwepo wa Mtandao wa Computer ili data zinazopatikana ziweze kuingizwa katika Server yaani Daftari kuu kwa wakati badala ya kutumia kutumia storage media kama flash memory kutunzia data zinazotakiwa kuingizwa katika Server.

 
 
soma zaidi chadema blog

JK apokea vitabu vya sayansi kwa shule za Sekondari vilivyochapishwa kwa msaada wa watu wa marekani





Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es salaam.
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maabara katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam ambako  pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa  na Watu wa Marekani. Wa kwanza kulia ni Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, akifuatiwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, na viongozi wengine wakiangalia jinsi somon la sayansi likifundishwa katika darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam 
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,na viongozi wengine wakisalimia wanafunzi katika   darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam 

soma zaidi hapa michuzi blog 

Wateja watatu Dar wakabidhiwa magari na Airtel baada ya kuibuka washindi

 
Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akishangiliwa na wafanyabiashara wenzake sokoni hapo, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana.





Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi mfano wa ufunguo wa  gari kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi, Grace Pascal Kalengela  wakati wa  kumkabidhi  gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni mume wa mshindi huyo, Daudi Mayunga na (kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
 
Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akiwa mwenye furaha, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.





Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akiwa mwenye furaha, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange


Wateja watatu Dar wakabidhiwa magari na Airtel baada ya kuibuka washindi
Dar es Salaam, Februari 24, 2015

MWANAMKE mchuuzi wa mboga mboga katika Soko jipya  la Kawe jijini Dar
es Salaam, Grace Pascal Kalengera, jana alikuwa miongoni mwa wakazi
watatu wa Dar es Salaam waliokabidhiwa zawadi zao baada ya kushinda
promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi.

Ijumaa iliyopita, soma zaidi

Monday, February 23, 2015

Mjue Dr. Slaa, msomi, mpole, mkarimu, mwenye busara na mwenye tabasamu la kudumu


Na Yericko Nyerere
Dr. Slaa si mtu mwenye maneno mengi, ni mtulivu na mkimya kiasi chake, mwenye tabasamu la kudumu, lakini akipanda jukwaani na kuanza kulishambulia huku na kule huwezi kuamini kinachotoka ubongoni mwake. Kimya kingi kina mshindo.

Wengi hawamfahamu Dr. Slaa vilivyo, wengi wanamwona sasa baada ya kuingia bungeni na sasa katika majukwaa ya siasa, ukweli ni mtu mbunifu, mpenda maendeleo na mwenye kujitoa kwa ajili ya wengine bila kujibakiza. Ufahamu wangu wa huyu Dr. Slaa ni wa muda mrefu, lakini wengi wetu wanachukulia mambo ya juu juu tu bila kujua undani na utendaji uliotukuka wa mtu huyu.

Machache kati ya mengi kuhusu Dr Slaa kabla ya kuwa Mwanasiasa na hatimaye kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, ana mlolongo wa mambo mengi ambayo yanaonyesha ubunifu wa hali ya juu, na pia mwepesi kuwaelewa vijana na kuendana nao tofauti na watu wengine wa kizazi chake.

Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM, baada ya kuombwa na Wanakaratu agombee ubunge kule baada ya kuchoshwa na mbunge aliyekuwepo wakati huo, CCM iliendelea na mizengwe ile ile kama ilivyo desturi ya chama hiki kuwakwepa watu wakweli, Wanakaratu wakiamua hawataki longolongo, wakamsihi kwamba wameamua awe mbunge wao na wakamwomba achague chama kingine agombee kwani hawamtaki kabisa mbunge aliyepo. Kwa ridhaa ya wananchi akaamua kujitoa CCM na kujitosa kujiunga na Chadema baada ya kuridhishwa na itikadi ya Chadema, akagombea ubunge kuridhia matakwa ya wanakaratu.

Kabla ya kuwa mwanasiasa
kuna mengi ya maendeleo ambayo wengi tunayaona huku tusijue kama Dr. Slaa ndiye aliyebuni na kuyaendesha kama ifuatavyo.


Dr. Slaa ndiye amekuwa wa kwanza Tanzania kuagiza big truck for load and unload makontena bandari ya Dar es Salaam wakati akiwa Katibu Mkuu TEC. Ilikuwa ni miaka ya 1980th, hakukuwa hata kampuni au watu binafsi waliothubutu kufanya hivyo. Truck hilo lilikuwa na crane za kupakia na kupakua bila taabu kokote linalokifkishwa container na kwa truck hilo. Baadaye makampuni yakabembeleza wauziwe gari ile, ndipo Barala La maaskofu likawauzia.
Kwa mara ya kwanza baraza la Maaskofu Tanzania lilipoanza kuwa na matumizi ya computer ikiwepo ofisi yake Dr Slaa kama katibu Mkuu, na taasisi za upashanaji habari ambazo zilikuwa chini ya uongozi wake ikiwa ni pamoja na:

Gazeti la kiongozi kuanza kutumia mfumo wa computer katika idara ya set up
TMP (Tanganyika Mission Press) Kipalapala idara ya uchapishaji (printing) wakitumia Apple computers.
TMP Book deparment Tabora mjini) idara ya maduka ya vitabu na usambazaji vitabu wakitumia Apple computers
TAPRI idara ya tungo za mawasiliano vitabu TEC iliyokuwa na ofisi zake Seiminari kuu Kipalapala Tabora.

Idara hizo zilikuwa na matumizi ya computer na PageMaker & QuakExpress software ambazo kwa graphic designers ilikuwa kitu kigeni kisichozoeka bado Tanzania ukitilia maanani wakati huo tulikuwa na chuo kimoja tu cha ardhi kule Tabora kujifunzia Graphic Design kabla ya Ardhi Dar haijaanza kukamilika. Huo ni ubunifu wa Dr. Slaa kwa wakati huo wakati wengi Tanzania hawajafunguka kuhusu matumizi ya teknologia ya ulimwengu wa dot com.


Wakati huo chuo pekee cha mawasiliano (journalism) Tanzania kilikuwa ni Nyegezi-Mwanza pekee kilichokuwa kikiongozwa na AMECA (Balaza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati kimoja kikiwa Kitwe - Zambia, cha Nyegezi kiliendeshwa na TEC Dr. Slaa akiwa msimamizi mkuu kama Katibu Mkuu.

Dr. Slaa atakumbukwa sana kwa makubwa aliyofanya kujenga na kuikuza TEC


Makao makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) tunayoona siku hizi ni matunda ya ubunifu wa Dr. Slaa alipokuwa Katibu Mkuu pale. Jengo la awali ni lile lililo upande wa mbele zinapotumika ofisi siku hizi ambapo yalikuwa madarasa ya shule ya sekondari ya Masisita Tanzania, ambayo baadaye ilihamishiwa Bigwa Morogoro kupisha kiwanja hicho kuwa makao ya Maaskofu Katoliki Tanzania, awali yalikuwa pale ofisi za St. Joseph, Dar es Salaam. TEC aliyoikuta DR. Slaa ilikuwa na jengo hilo la madarasa na jengo lilolokuwa la utawala wa shule. Dr. akabuni majengo ambayo tunayoana sasa, hata kama hayakukamilika yote waliofuata walikamilisha kazi alioyoianza.
Kaone maendeleo na majengo katika jimbo la Mbulu ni jitihada za Dr. Slaa na Fr. Narda ambao kwa pamoja walifanya makubwa.
Kaangalie jimboni kwake huduma za kijamii ambazo amezifanya, utachoka mwenyewe kiasi ambacho CCM imekimbiwa kabisa huko sababu utendaji wa Slaa huko na CCM ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu.
Dr. Slaa kwa tunaomfahamu ni mwanamapinduzi na mpenda maendeleo, na pengine mengi alikuwa anayafanya yakaonekana mapya mno kwani alikuwa anaona mbali kuliko hawa wakubwa wake, ila sipendi kuliongelea sana hilo.

Chadema yaimarika baada ya Dr. 

Ndani ya Chadema Dr Slaa akiwa katika kiti cha Mtendaji mkuu amefanya mageuzi mengi sana, ni mtendaji mkuu wa Upinzani pekee aliyeweza kuhimili mikikimikiki ya ya udgarimu wa serikali ya ccm inayotumia vyombo vyake vya dola kukandamiza upinzani, Moja ya mageuzi makubwa na yakutuka aliyoyafanya Dr Slaa ni kuunda idara imara ya ulinzi ya chama ambayo kwa liasi kikubwa imefanikiwa kukidhoofisha chama tawala ambapo kwa upepo huu mwezi wakumi upinzani utachukua dola rasmi.


Siyo siri Chadema hakikuwa na nguvu tunayoona sasa hivi licha ya kuwa na sera nzuri, lakini leo tunaona nguvu ya Chadema inayoogopewa mno na CCM ni kutokana na Chadema katika dakika za majeruhi kuamua kumwangukia Dr. Slaa agombee urasi ambao Samweli Sitta aliingia mitini baada ya makubaliano nao. Tangu hapo Chadema imekuwa na nguvu ya ajabu.

Je, vijana hao waliokuwemo ndani ya Chadema kabla ya Dr. Slaa kugombea Urais kwa nini hawakuipaisha juu Chadema kama sasa? Baada ya Dr. Slaa kuipaisha Chadema juu sasa tunakuja na kauli mbiu ya kubeza makubwa yaliyofanywa na hawa mnaowaita kizazi cha kabla ya uhuru. Hapana tuwe waungwana, pamoja na kila mmoja kuwa na haki za kugombea nafasi tusigeuze uhuru huo kuwabeza hawa ambao wametufikisha tulipo, na bado tunahitaji mchango wa ushauri, uongozi, hekima na busara zao. Uongozi bora ni kuchanganya mapya na ya kale kwani viatu vya zamani vyaijua njia.
Ubunifu wa Chadema viongozi wakiwa mojawapo waliozaliwa kabla ya Uhuru Dr Slaa na Kamanda Mbowe:

Dr. Slaa ndiye mbunge ambaye baada ya kuingia bungeni alianza kuchangamsha kwa kuichambua serikali na kasoro zake kitu ambacho katika mabunge yaliyotangulia wabunge walikuwa ni rubber stamp ya serikali.

Chadema wakiwemo hao unaoona walizaliwa kabla ya uhuru wamebuni mapya katika shughuli na kampeni za uchaguzi Tanzania kuwa zenye mvuto kuanzia mkuktano wa ufunguzi wa kampeni uchaguzi Mkuu uliopita ulifanyika Kidongo Chekundu baada ya Dr. Slaa kushusha makumbora mazitomazito kuituhumu serikali, watendaji wa serikali na CCM, tuhuma ambazo CCM wanazidi kubabaika kuwanyoshea kidole wahusika kisha kuwakumbatia tena hivi karibuni kule Dodoma.

Mkutano wa Kidongo chekundu Dar es Salaam ndio ulioanza kutufungua macho na masikio Watanzania na kuanza kujifunza elimu ya uraia ambayo tulikuwa tunazibwa na CCM tusiijue.
Dr. Slaa ndiye aliyetufunza na kutufunua kwamba raia wanayo nguvu ya kuiadabisha serikali haki zao za msingi zinapokiukwa kwa kauli mbiu ya nguvu ya umma (peoples power).
Utumiaji wa chopper kufikia maeneo magumu kufikika kwa magari na kurahisisha kazi ya kampeni, CCM wakaiga.
Kuwa na magari yanayotumika kama majukwaa ya mikutano badala ya kupoteza gharama na muda kujenga majukwaa yatakayotumika kwa dakika chache.

Ilani ya Uchaguzi Chadema 2010 ndiyo inayotumika na yenye uzito sasa hivi:

Fukuto la Katiba mpya linaloendelea sasa nchini ni uzao wa ilani ya Chadema na ilani ya Dr Slaa kwamba kinachofuata baada ya Uchaguzi mkuu ndani ya siku 10
Kikwete kufanya mabadiliko ya barala la mawaziri mara kadhaa ni kutokana na shinikizo la wabunge wa Chadema bungeni.

Kuna mengi tu wachangiaji wengine watachangia, ni dhana potovu kuwa na fikra za aina hiyo na kuwabeza wabunifu wa mengi, waliongoza nchi hii, wenye kuturithisha mengi kwa uzoefu na busara zao na walioongoza nchi hii hadi kuwa na utulivu wa aina yake. Leo vijana mnaowasema yanayojilia ni amani kusambaratika na mauaji ambayo ilikuwa hadithi za kusimuliwa kutoka nchi nyingine, leo serikali ya CCM inayoongozwa na Rais aliyechaguliwa kwa tiketi ya kupumbazwa umma ya kijana kuliko Rais mwingine aliyemtangulia imetwishwa na aibu kubwa ya kitaifa na kimataifa ya mauaji ya raia wasio na hatia.

Kuna nchi ambazo ni kielelezo cha vijana ambao mimi ningewaita watoto kukabidhiwa madaraka ya kuongozia nchi na kusababisha maafa makubwa kwa nchi husika kama Liberia, Ujerumani chini ya Hittler,

Vijana achaneni na uroho wa madaraka, vema kubaki watumishi na watendaji wazuri serikalini na vyamani kujifunza mbinu za uongozi na kupata uzoefu katika kuongoza nchi.

Kuongoza nchi hakuna shule wala kitabu cha kusomea au chuo. Hekima na busara ya mtu ndio kielelezo cha fanaka katika kuongoza nchi.

Vijana wana papara,
wanataka njia ya mkato,
pagumu wanataka kulazimisha bila busara wala kutumia akili
Vijana wanalipuka kama moto wa gas
mambo yakigeuka magumu ni mabavu hutumika


Chanzo CHADEMA BLOG        

Friday, February 20, 2015

MAKAMU WA RAIS DK. MOHAMED BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

 

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akimkabidhi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid machapisho mbalimbali baada ya kuzindua kongamano la siku mbili la kimataifa la watoto walio katika mazingira hatarishi Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.

 
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akimkabidhi Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba machapisho hayo.

 

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki machapisho hayo kwa niaba ya wakuu wote wa mikoa.

 
Mratibu wa Ulinzi na Usalama wa Mtoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (Unecef), Mbelwa Gabagambi, akizungumza katika hafla hiyo.

 
  Mwakilishi wa watoto, Coletha Emanuel kutoka mkoani Shinyanga akisoma hutuba yao mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal.
 
Wadau wa maswala ya watoto wakiwa kwenye kongamano hilo.

 
Watoka kutoka mikoa mbalimbali wakiwa kwenye 
kongamano hilo.
 
 
Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi wa kongamano hilo.
 
 

Nini Wanafunzi wafanye Baada ya Matokeo Ya Kidato cha Nne



Huzuni ikipitiliza humpelekea mtu kukata tamaa na kutoona thamani ya maisha na hata kufikia hatua ya kunywa sumu au kujiua wakati furaha ikizidi humfanya mtu akasahau majukumu mengine mazito yaliyo mbele yake.
Matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka hivi karibuni yamewaacha wanafunzi na wazazi wengi kwenye majonzi huku wengine wakiwa na furaha. Hii ni kutokana na idadi ya wanafunzi waliomaliza kuwa na matokeo ya wastani katika mitihani yao.
Pamoja na hilo, kubwa ni kuangalia namna bora ya kusonga mbele kwa wale ambao hawakufanya vema wakijipanga upya kuangalia ni yepi ya kufanya ili kuweza kusonga mbele baada ya jitihada zao zilizotangulia kutofanikiwa wakati wale waliofaulu vizuri wakiweka mipango na mikakati madhubuti itakayowawezesha kuendelea zaidi.  
Jambo la kwanza analopaswa kulitambua mwanafunzi ni kukubali matokeo aliyoyapata. Kuukana ukweli huu hakutakuwa na msaada kwake. Ni wazi zinaweza kuwapo kasoro za hapa na pale katika masuala ya usahihishaji lakini mchango wake katika matokeo ya jumla unaweza usiwe mkubwa sana.
Kwa muhtasari, matokeo ya kidato cha nne unaweza kuyagawa katika makundi yaliyopangwa katika Muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Points Average ama GPA) ambayo ni daraja la ‘A’ kundi la fauli Uliojipambanua (Distinction) litakuwa na alama kati ya 3.6-5.0, ‘B’ Kundi la Kundi la ufaulu mzuri (Merit) litakuwa na alama kati ya 2.6.3.5, ‘C’ kundi la ufaulu wa wastani (Credit) litakuwa na alama kati ya 1.6-2.5, ‘D’ Kundi ufaulu hafifu (Pass) 0.3-1.5 na ‘F’ Kundi la ufaulu usioridhisha (Fail) 0.0-0.2.
 
Aidha unaweza kuyagawa katika makundi manne ya walio na sifa za kuendelea na kidato cha tano na vyuo vya ufundi; wasio na sifa za kuendelea na kidato cha tano na vyuo vya ufundi lakini wana fursa za kuendelea na vyuo vingine; na waliofeli kabisa amabo wanakosa sifa za kuendelea na masomo kwa vigezo vya ufaulu wa kidato cha nne.

Kujiunga kidato cha tano na vyuo vya ufundi
 
Awali ya yote ifahamike kuwa wanafunzi wanaochaguliwa moja kwa moja kujiunga na kidato cha tano au vyuo vya serikali ni wale wanaotoka shuleni (school candidates) na si watahiniwa wa kujitegemea (private candidates).
Kadhalika wanafunzi wanaochaguliwa moja kwa moja katika vyuo vya ufundi mfano Dar es Salaam Institute of Technology (DIT), Arusha Institute of Technology (AIT) na kama hivyo, huwa na sifa sawa na wale wanaochaguliwa kuijunga na kidato cha tano katika michepuo ya sayansi. Idadi ya wanafunzi hawa huwa si kubwa sana.
Mwanafunzi aliyefaulu kwa Distiction na Merits ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano au chuo cha ufundi katika shule na vyuo vya serikali. Aidha hata waliopata Credit na Pass wana nafasi ya kuchaguliwa. Si tukio la kawaida mwanafunzi aliyepata divisheni F kuchaguliwa kujiunga kidato cha tano au chuo cha ufundi.
Mara nyingi changamoto wanayokuwa nayo wanafunzi waliofaulu kwa viwango vya juu ni aina ya michepuo na shule za kuendelea nazo. Ni jambo la kawaida kukuta kijana akifaulu masomo mengi na kisha kusoma mchepuo ambao hana mapenzi nao sana. Hili husababishwa na mazingira ya ujazaji fomu za michepuo ya kuendelea nayo baada ya kuhitimu masomo. Hutokea kuwa mchepuo anaoupenda sana ana shaka ya kufanya vizuri na hivyo kuchaguwa michepuo mingine. Ama kwa upande wa shule, hutegemeana na nafasi, ufaulu wa wanafunzi na idadi ya wanafunzi walioomba katika Shule husika. 


Baadhi ya wanafunzi wanapokosa michepuo au shule walizoomba huhangaika na kutumia muda mwingi wakitaka kubadilisha. Uzoefu unaonyesha kwamba ni sehemu ndogo za sana ya wanafunzi hao ambao hufanikiwa. Ushauri wetu ni kwamba endapo kijana atachaguliwa katika shule asiyoipenda na hakuna sababu za kiafya za kumfanya asiende katika shule hiyo pengine kutokana na hali ya hewa, au kachaguliwa mchepuo asioupenda na familiya yake haina uwezo wa kumsomesha shule binafsi, basi atulizane katika hicho alichopata na ajikite zaidi katika masomo kwani anaweza pia kufanikiwa katika fursa hiyo aliyoipata.
Changamoto nyingine ambayo huwakuta vijana wa kundi hili ni kuanza kusoma tuisheni za masomo ya kidato cha tano kabla ya uchaguzi kufanyika. Utata wa jambo hili ni kama tulioueleza hapo juu wa mwanafunzi kuchaguliwa mchepuo tofauti kabisa na masomo anayosoma. Kwa mfano kuna kijana tunayemfahamu akisoma masomo ya mchepuo wa Economic, Geography na Mathematics (EGM) lakini akachaguliwa mchepuo wa History, Kiswahili na Language (HKL). Tofauti iliyoje! Katika hilo inashauriwa kuwa kama mwanafunzi hana hakika ya kusoma katika shule binafsi, asianze masomo hayo mpaka baada ya uchaguzi wa kidato cha tano kufanyika. Na ikibidi kujisomea asome vitu vya jumla kama masomo ya lugha, kompyuta nk. 
Kwa wale waliokwisha amua au lazima wasome katika shule binafsi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya ubora wa shule hizo kitaaluma, maadili na stadi nyingine za maisha. Aidha ni muhimu kufuatilia juu ya kiwango cha ada, muda wa kuchukuwa na kurejesha fomu za maombi, tarehe ya usaili na ya kufungua shule. Hutokea mwanafunzi akapoteza muda na hatimaye kuhangaika kutafuta shule wakati shule nyingi zimeshasimamisha kupokea wanafunzi. 
 
Kuna wanafunzi waliopata Pass na Credit ambao hawatapata nafasi ya kujiunga na kidato cha tano. Hata hivyo vijana waliopata Pass na sehemu ndogo ya waliopata Credit huwa wanapata sifa na wanaweza kujiunga na kidato cha tano katika shule binafsi endapo uwezo wa familiya unaruhusu. Hii ni kutokana na kanuni za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo zinamruhusu mwanafunzi kuendelea na masomo ya kidato cha tano endapo amefaulu katika kiwango cha angalau alama C kwa masomo matatu au zaidi hata kama masomo aliyofaulu hayatengenezi mchepuo wowote mfano Civics, Biology na English huku akiwa amepata alama D au chini yake katika masomo mengine. Endapo familiya itamudu kumsomesha kidato cha tano kati shule binfasi, ni vema kijana akapata ushauri wa wazazi, walimu na wazoefu wengine juu ya mchepuo stahiki inayomfaa. Mara nyingi wanafunzi wa aina hii huwa wanashindwa kutofautisha baina matashi ya nafsi na uwezo binafsi wa kimasomo. Kwamba kijana tuliyemtaja hapo juu asome CBG au HGL ni suala linalohitaji tafakuri pamoja na mhusika.
Kujiunga na vyuo vya Ualimu
 
Kuna wanafunzi waliopata Pass na hata Credit ambao hawatachaguliwa kujiunga na kidato cha tano lakini watachaguliwa kujiunga na vyuo vya ngazi ya Diploma mfano vyuo vya Ualimu. Kwa mujibu wa kanuni zilizopo sasa, kiwango cha ufaulu cha mwisho kuchukuliwa ni Credit. Pamoja na kujaza nafasi za masomo ya Ualimu, mwanafunzi atapaswa kuomba rasmi nafasi hizo kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi au katika vyuo binafsi baada ya matokeo kutoka na nafasi kutangazwa rasmi. Aidha kutokana na uchache wa nafasi katika vyuo huwa si wote walio na sifa wanaoweza kuchaguliwa serikalini lakini nafasi ni nyingi sana katika vyuo binafsi.
 
Kujiunga na Vyuo Vingine
 
Wapo vijana ambao licha ya kuwa na sifa za kuchaguliwa katika vyuo vya ualimu, huwa hawachagui au hawaendi hata baada ya kuchaguliwa kwasababu zao binfasi. Kama uwezo wa familia unaruhusu na mnaona kusoma ualimu si kipaumbele chenu haina tatizo. Hata hivyo, ni vema kuangalia fursa zilizopo na uwezo wa familia kiuchumi. kijana anapaswa kufahamu kufahamishwa kuwa si busara kwa familia yenye uwezo duni wa kiuchumi, kama zilivyo familia nyingi za kitanzania, kumsomesha kijana katika ngazi hii kwa gharama kubwa wakati kuna wengi wanahitaji kuendelezwa kitaaluma katika familia.
Wale wote waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi, vyuo vya kawaida au vyuo ualimu, fursa pekee waliyonayo ni kujiunga na vyuo vingine vinavyotoa kozi mbalimbali kama, biashara, utawala, ufundi, nk. Vyuo kama College of Business Education (CBE), Tanzania Institute of Accountancy (TIA), Institute of Social Work (ISW), Institute of Information Technology (IIT) ni mifano michache katika ya vyuo vingi vilivyopo. Changamoto kubwa katika vyuo hivi ni uwezo wa kuzimudu gharama zake za mafunzo hayo. 
Mwanafunzi aliyefeli kabisa na kupata Sifuri (0), hana fursa yoyote katika zote zilizotajwa hapo juu. Hata hivyo anakuwa amepata cheti cha kuhudhuria masomo (leaving certificate) ambacho huwa na msaada fulani katika maisha kwa kuna wakati huhitajika vijana waliomaliza kidato cha nne bila kujali ufaulu wake. 
Pia kuna fursa zinazohitaji vijana waliomaliza shule ya msingi ambazo bado zinaweza kutumiwa na vijana hawa. Kwa mfano kuna fani mbalimbali zinazotolewa na vyuo vya VETA kama ufundi, udereva, usafi,utunzaji bustani, upishi nk ambazo zinaweza kutumiwa vema na vijana ambao hawakufaulu mitihani ya kidato cha nne.
Ni muhimu kutaja hapa kwamba si waliofeli tuwanaoweza kuzitumia fursa za mafunzo ya VETA bali hata wale waliopata divisheni Pass na hata Credit ambao ama hawakupata fursa za kuchaguliwa kidato cha tano au familiya zao hazimudu kuwasomesha katika shule au vyuo vya kujilipia. 
 
Kurudia Mitihani

Wanafunzi wengi wanaofanya vibaya katika mitihani yao, jambo la haraka linalowajia vichwani ni kurudia mitihani. Ndio maana siku hizi vituo vinavyotoa mafunzo kwa wanaorudia mitihani vimekuwa vikiongezeka kila kukicha. Ni kwakuwa soko linakuwa na wateja wameongezeka.
Pamoja na kuunga mkono na kuheshimu juhudi za wanaotoa mafunzo hayo, tungependa tutanabahishe kwamba ni ili kuepusha upotevu mwingi wa muda na pesa, ni vema mwanafunzi akawa akijiandaa kurudia mitihani huku akijufunza ujuzi mwingine. Uzoefu unaonyesha kuna wanafunzi wanaorudia mitihani na matokeo yao kuwa mabaya kuliko ya mwaka uliotangulia. Aidha kuna wanafunzi waliorudia mitihani zaidi ya mara moja na bado hawakufanikiwa kupata alama C au zaidi (credits) tatu walizohitaji ili wajiunge na kidato cha tano.
Endapo mwanafunzi atajiandaa kurudia mitihani huku anapata ujuzi mwingine mfano udereva, ufundi,nk anakuwa katika nafasi nzuri ya ajira hata asipofaulu mitihani yake anayorudia. Ni uzuri ulioje endapo atapata vyote - credits na huku ana cheti cha ujuzi wake. 
Jambo hili linawezekana endapo kijana ataugawa vizuri muda wake chini ya muongozo wa familia kwa mfano asubuhi akienda chuoni kupata ujuzi na jioni akienda tuisheni kwa ajili ya kurudia mitihani. Aidha endapo mwanafunzi hatofanikiwa kupata credits, anaweza kuanza kazi huku ajiandaa taratibu kurudia mitihani yake. Wengi wamefanikiwa kwa utaratibu huu.
Kukata rufaa juu ya matokeo
Wapo wanafunzi ambao wanakuwa hawakuwa hawakuridhika na matokeo waliyopata wakiamini hawakutendewa haki katika usahihishaji pengine kwa kuzingatia rekodi za matokeo yao katika mitihani ya shuleni au kwa jinsi walivyofanya mitihani. 
 
Kwamba hatupingi jambo hili ndivyo pia tungependa kusisitiza kuwa wakati ukikusudia hilo ni vema ukaendelea na mipango mingine ya kujiendeleza kama tulivyoitaja hapo juu. Hii ni kwasababu ni wanafunzi wachache sana ambao matokeo yao hubadilika baada ya mitihani yao kusahihishwa upya. Aidha unaweza kupoteza muda mwingi ukisubiri hatma ya rufaa yako na kisha majibu kuja usivyotarajia. 
Ufadhili wa Masomo
 
Hutokea wanafunzi waliopata nafasi za masomo katika shule binafsi au vyuo vinavyohitaji kujilipia wakawa hawana uwezo wa kujisomesha na hivyo kuhangaika huku na kule kutafuta ufadhili. Ukweli ni kuwa ni wachache sana ambao hufanikiwa. Hii ni kutokana na kutokuwa na taasisi rasmi zinazotoa ufadhili katika viwango hivi ya elimu nchini.
Pamoja na kutokatishana na tamaa,  ni vema mtu unapokuwa katika hali hiyo kutafuta shughuli itakayokuwezesha kujenga nguvu za kiuchumi na kisha kuweka akiba kwa ajili ya kujisomesha. Unaweza kuweka malengo ya kusoma huku ukifanya kazi. Endapo shughuli zako hazikupi fursa ya kusoma huku ukifanya kazi, unaweza kuahirisha kusoma hadi kipindi fulani baada ya kujiimarisha kiuchumi. Endapo hilo litakuwa gumu kulitekeleza, familia iangalie uwezekano wa kuuza sehemu ya rasilimali endapo inazo na ambazo hazitaithiri familia nzima endapo zitauzwa.
 
Tuhitimishe kwa kusema, matokeo vyovyote yawavyo hayawezi kuwa ndio mwisho wa maisha. Siku zote wanaofanikiwa ni wale wanaotazama mbele huku wakijifunza kwa yaliyowatokea. Walofaulu washukuru huku wakijipanga; waliofanya vibaya wasubiri huku wakijifuza. Tumia vizuri kila fursa unayoipata bila kujali udogo wake. Jifunze kwa wengine, uliza, pata miongozo kwa waliokutangulia, na amini kuwa ipo siku ufanikiwa. Washindi hawaachi, na wenye kuacha hawashindi.
KUVUNJIKA KWA KOLEO SI MWISHO WA UHUNZI
Kwa Msaada zaidi wa ushauri na namna bora ya kusoma tafadhali wasiliana nasi kwa namba 255 767 488856
au barua pepe marshk86@hotmail.com 
 
 
Chanzo ni mbeyayetu
 
 
 
 

 

Wednesday, February 18, 2015

TAARIFA YA UPIMWAJI NA UUZWAJI WA VIWANJA KATIKA MJI WA CHALINZE


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1Zf_-IWnK_pDOSykTYu9ND5wguLoUbCE4jP0mE1q4Guiv9l4jn0YsmqWLZiJDymizrQqfAYmswwzRS_xi2trsbV9KDrGttI7UWkLQxQWPoGFvg6boeP-zzmHXKvLL1G8Dt-hv2HdcSjA/s1600/Screen+Shot+2015-02-18+at+11.12.49+AM.png
Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya miradi ya maendeleo ya miundombinu iliyochini ya wizara ya fedha anautangazia umma juu ya upimaji na uuzwaji wa viwanja katika mji wa chalinze

Fomu za maombi zinapatikana katika matawi ya benki ya posta ya Azikiwe kwa mkoa wa dar es salaam na benki ya posta bagamoyo na chalinze kwa mkoa wa Pwani.

Pia maombi yanaweza kufanyika katika tovuti yetu ya

www.utt-pid.org

TAARIFA KUTOKA JWTZ

 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa ya kifo cha Askari wake Praiveti Ahadi Mwaka Mwainyokole kilichotokea tarehe 4 Februari 2015 katika mji mdogo wa Mbalizi, Mkoani Mbeya.

Taarifa za mazingira ya kifo cha Askari huyo zimepotoshwa na baadhi ya Vyombo vya Habari na kusababisha mapokeo tofauti kwa wananchi.

Hali halisi ni kwamba, mnamo tarehe 4 Februari 2015 Askari huyo akiwa na Askari wenzake wanne (4) ambao ni Koplo Bedatu Benard Mloka, Praiveti Thani Hamisi Haji, Praiveti Mzee Buan Mzee na Praiveti Mohamed Juma walivamiwa na kundi la wahuni wakati wakitoka matembezini. Chanzo cha vurugu hizo ni kutokana na Praiveti Rashid Maulid wa Kikosi chao kuibiwa samani kwenye nyumba aliyokuwa amepanga uraiani katika mji mdogo wa Mbalizi, Kitongoji cha Shigamba. Samani alizoibiwa ni pamoja na TV aina ya LG “flat screen” “Inch 20”, radio aina ya Sony moja, Deck aina ya Sangsung, flash moja, extension cable moja na fedha taslimu Tshs 30,000/=.

Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi tarehe 03 Februari 2015 na kupatiwa RB yenye Nambari MBI/RB/285/2015, sambamba na kutoa taarifa Polisi. Kituo hicho cha Polisi kilitoa askari mmoja ambae aliungana na askari Jeshi na wenzake na wakaenda eneo la relini ambako vijana wasio na ajira maalumu hushinda. Waliwakamata vijana saba, mmoja wa vijana hao alikimbia na kwenda kuwapa taarifa wenzao ambao hawakuwepo katika eneo hilo ambapo vijana sita walifikishwa kituo cha Polisi.

Ilipofika saa tatu usiku askari hao wakiwa katika matembezi ya kawaida walikutana na kundi la vijana wakiwa na silaha mbalimbali kama nondo na marungu ambao walianza kuwashambulia huku wakiwashutumu kuwa waliwapeleka wenzao Polisi.

Kwa kuwa kundi la vijana hao lilikuwa kubwa na likiwa na silaha zilizotajwa lilifanikiwa kuwajeruhiAskari hao akiwemo Praiveti Ahadi Mwainyokole ambae alijeruhiwa vibaya.
Askari hao walikwenda Polisi na wakachukuwa PF3 na kisha kwenda katika hospitali ya Jeshi Mbeya baadaye Praiveti Mwainyokole alifariki muda mfupi baada ya hali yake kutokuwa nzuri kutokana na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyosababisha damu kuvia kwenye Ubongo.

JWTZ linasikitishwa na mauaji hayo yaliyofanywa kwa Askari wake, na mauaji ya askari wengine katika maeneo ambako vitendo kama hivyo vimetokea. Ikumbukwe kuwa JWTZ lipo kwa ajili ya usalama na ustawi wa wananchi, hivyo JWTZ linalaani vitendo viovu vinavyofanyika kwa askari wake na linatoa rai kwa vyombo vya sheria kuchukua mkondo wake.

Kimsingi JWTZ halina ugomvi na wananchi kwani kazi yake ya msingi ni kuwalinda ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kimaendeleo kwa utulivu na amani kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.

Imetolewa na
 Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga