Kuna faida nyingi za kujenga mwili wako zinazotokana kwa kula matunda. Licha ya kupenda ladha tamu za matunda mbalimbali, matunda yana virutubisho vingi kama vitamin na madini. Vitamin A na C hupatikana kwenye matunda mengi ukilinganisha na virutubisho vingine vilivyopo kwenye matunda ya aina mbalimbali.
Matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo( heart diseases ), stroke (kiharusi ), shinikizo la damu ( blood pressure ), cholesterol, aina mbalimbali za saratani (cancer ), matatizo ya uwezo wa macho kuona na mengine mengi.
Matunda yote yana manufaa mwilini kwa afya lakini napenda ujue faida kadhaa zinazopatikana kwenye apple, parachichi, ndizi, zabibu, embe, chungwa, papai na nanasi.
Zijue faida mbalimbali zitokanazo kwa kula matunda yafuatayo
1. APPLE
Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari ( diabetes ) na pumu (asthma )
Husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya ( natural mouth fresher ) vilevile apple husafisha meno unapotafuna.
Harufu nzuri ya apple hupatikana kwenye maganda/ngozi yake, hivyo ni vyema ukalitafuna pasipo kulimenya kwani vitamin nyingi pia hupatikana kwenye maganda/ngozi ya juu ya apple.
2. PARACHICHI
- Ni chanzo cha vitamin E.
- Hupunguza kiwango cha cholesterol mwilini kwakuwa halina mafuta mengi sana ukilinganisha na nyama au mbegu zitoazo mafuta.
Watoto hupenda sana kula parachichi kwasababu ni laini na pia mafuta ya parachichi husaidia katika kukuwa vizuri kwa mtoto na kuwa mwenye afya bora.
3. NDIZI
- Ni chanzo cha vitamin B6 na madini ya potassium.
- Licha ya kuwa na ladha nzuri, ndizi zina madini mengi ya potassium ukilinganisha na matunda mengine ambayo husaidia kupunguza ongezeko la shinikizo la damu ( blood pressure ).
4. ZABIBU
- Ni chanzo cha madini ya manganese.
- Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa kusaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu ( blood pressure )
- Huepusha magonjwa ya aina mbalimbali za saratani kwa kuzuia usambaaji wa seli za saratani ya titi ( breast cancer ), tumbo ( stomach cancer ) na utumbo ( colon cancer ).
5. EMBE
- Ni chanzo cha vitamin A na E.
- Vitamin A iliyopo kwenye embe husaidia kuboresha macho yako kwa kukuwezesha uweze kuona vizuri. Pia husaidia kupunguza uwezekano wa kupata upofu kwa wazee kwa kuimarisha macho.
6. CHUNGWA
- Ni chanzo cha vitamin C na madini ya potassium.
- Chungwa lina vitamin inayojulikana kama ‘’folate’’ ( B-Group Vitamin ) ambayo husaidia katika kujengeka kwa ubongo wa mtoto kwa mama mjamzito.
- Chungwa lina kemikali zinazojulikana kama ‘’hesperidin’’ ambazo hupunguza kiwango cha cholesterol kwenye damu.
7. PAPAI
- Ni chanzo cha vitamin A na C.
- Papai lina enzyme ijulikanayo kama ‘’papain’’ ambayo husaidia katika usagaji au mmeng’enyeko wa chakula.
- Pia vitamin A iliyopo kwanye papai husaidia husaidia kuboresha afya ya ngozi yako.
8. NANASI
- Nanasi lina enzyme asilia ijulikanayo kama ‘’bromelain’’ ambayo husaidia kuvunjavunja protini hivyo husaidia katika mmeng’enyeko au usagaji wa chakula.
- Vilevile enzyme ya bromelain husaidia kupunguza ukuaji wa seli za saratani na kuchochea uponaji wa vidonda kwa haraka.
No comments:
Post a Comment