Wednesday, July 1, 2015

Matokeo ya Uchaguzi wa Kujiunga na kidato cha Tano Julai 2015.




OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015.Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansina Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomo ya sanaa na biashara..
bofya HAPA kupakua matokeo

Wednesday, June 24, 2015

SUGU ASHINDA KESI DHIDI YA MAMA MTOTO WAKE FAIZA, MAHAKAMA YAAMUA APEWE MTOTO




Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ameshinda kesi aliyomfungulia aliyewahi kuwa mchumba wake Faiza Ally ambaye pia ni mama wa mtoto wake wa kike aitwaye Sasha.
Kwa mujibu wa maelezo ya Faiza kupitia akaunti yake ya Instagram, mahakama imetoa hukumu ambayo ni mtoto achukuliwe na kulelewa na baba yake mzazi.
 Sugu alimshitaki Faiza kwa madai kuwa hana maadili na ana hofia kuwa atamharibu mtoto wao, hivyo alitaka kumchukua mtoto kutoka kwa mama yake aishi naye.


Hiki ndicho amekiandika Faiza baada ya hukumu kutolewa:
“SIELEWI JOSEPH AMESHINDAJE KESI- USHAHIDI WA PICHA PEKE YAKE SIONI KAMA UNATOSHA MIMI KUPOKONYA MTOTO WANGU- MTOTO WANGU NI MDOGO SANA ANANIHITAJI SANA – NA SITA RUDI HATA IKIBIDI KUUZA KILA NILICHO NACHO KWA AJILI YA KUSIMAMIA HILI- SIJAPEWA NAFASI NIMEPELEKWA MAHAKAMANI IJUMAA NA LEO JUMANNE NIMEPEWA HUKUMU/ MWANANGU ACHUKULIWE….. HAPANA ! SITARUDI NYUMA NA HAITAKUA RAHISI NINAKATA RUFAA NA KUTAFUTA WAKILI WA KUNISIMAMIA HILI- MWANANGU ANASOMA VIZURI ANAISHI VIZURI NA NAAMINI KWENYE MIKONO YANGU YUKO SALAMA ZAIDI YA KOKOTE/ YAANI KUHUSU KUKOSA KUKAA NA MWANANGU NI BORA KUFA KULIKO KUISHI NIKIMUONA SASHA ANA LELEWA NA MAMA MWINGINE IKIWA MIMI MAMA YAKE NIKO HAI NA MAKINI KATIKA MALEZI YA MTOTO WANGU- NINA NDOTO NA MWANANGU NYINGI SANA – NAHITAJI KUISHI NAE YEYE NDIO KILA KITU KWENYE MAISHA YANGU/ NAMPENDA SANA MWANANGU NA SIJASHINDWA KUMLEA- NAONA UCHUNGU SANA KUPELEKEA MAHAKANI NA KUPOKONYWA MTOTO WANGU BILA SABABU ZA MSINGI . SITAOGOPA CHEO CHAKE CHA UBUNGE KAMWE- NTASIMAMA KAMA MAMA MWENYE HAKI KWA MTOTO WAKE …MUNGU NAOMBA NIELEKEZE.NISIMAMIA NA UNIHUKUMIE HUU UKATILI NINAO FANYIWA NA BABA SASHA …..”

TAARIFA KWA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA: ENDESHA POLEPOLE CHOMBO CHAKO CHA MOTO KONA YA MBEYA HOTEL KAMA UNAELEKEA MWANJELWA KUNA MATUTA.



Mafundi wakiendelea kuweka Matuta kona ya kushuka kilima cha Mbeya Hotel kuelekea Mwanjelwa na maeneo mengine
 
 Hapa Lift Valley pia pana tuta punguza mwendo
  

 

 
Picha zote kwa Hisani ya mbeyayetu.blogspot.com 

NECTA YATOA RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2015,SOMA IKO HAPA











Bofya Hapa kupata Ratiba

Tuesday, June 2, 2015

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Kimataifa, Bernard Membe, amewaomba Watanzania kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Membe amesema, amepanga kutangaza nia hiyo,  Juni 6, mwaka huu,  na kuwaomba wananchi wamsikilize kwa makini siku hiyo kwakuwa ataeleza kwa kina nini anataka kufanya nchi iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo.

Waziri Membe ambaye hajatangaza rasmi nia yake ya kuwania Urais, lakini ambaye ni miongoni mwa wanaotarajiwa kutikisa katika kuwania kiti hicho, alitoa mwito huo jijini Dar es Salaam jana,  katika Tamasha la Qaswida lililofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa.

“Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa nchi ni ule wa kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, suala la uadlifu ni lazima kupewa kipaumbele kwa viongozi alisema,” alisema Waziri Membe

"Ninawapongeza sana, kwa kuamua kuwajenga vjana katika maadili ya dini, msingi huu ndio unaoweza kuifanya Tanzanaia kuwa na viongozi walio bora kutokana na hofu ya Mungu, maana mtu asiye mchamungu hawezi kukosa kuwa mla rushwa, fisadi na mtumiaji mbaya wa madaraka" alisema Membe.

Membe alitumia nafasi hiyo kuwatahadharisha kuwa makini katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, kuacha kuchagua viongozi ambao kwa nje, wanajinadi  kuwa wachamungu, lakini matendo yao hayaendani na maadili ya  dini zao.

Alisema moja ya dalili za viongozi wasiokuwa waadilifu kwa kutokuwa na uchamungu huwa ni kusaka uongozi kwa kutumia fedha nyingi hivyo amewasihi wasiwachague viongozi wa aina hiyo wanaosaka uongozi kwa kutoa rushwa.

“Msikubali kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi kuwa na dini kinyume na matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu jambo ambalo limekuwa likisisitizwa na dini zote. Uongozi wa heshima ni ule unaochukia rushwa ambayo ni adui wa haki", alisema Membe.

Kuhusu tamasha hilo, Waziri Membe alipongeza uwepo wake ambapo ni kuwalea vijana katika maadili mema ya kumjua Mungu na kusema anajivunia Taasisi za aina hiyo.

Tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, zaidi ya vikundi 50 vimeshiriki tukio hilo la aina yake.

Akizungumza katika Tamasha hilo, Mkurugenzi wa Ulamaa Promotion Center ya jijini Dar es Salaam, Jumanne Ligopora, alihimiza umuhimu wa kila mtu kuwa sehemu ya ulinzi wa amani na utulivu.

Mwishoni mwa Tamasha hilo, Membe,  alikabidhi tuzo kwa watu mbalimbali na pia Membe mwenyewe kupewa tuzo kutokana na kutambua mchango wake katika masuala ya kijamii.

Hotuba ya Profesa Mark James Mwandosya aliyoitoa wakati wa kutangaza Nia ya kugombea uraisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

 
Profesa Mark Mwandosya akizungumza na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani waliojitokeza kumsikiliza akitangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM
 
Katibu wa siasa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi akimkaribisha Prof Mwandosya kutangaza nia
 
Vijana toka Zanzibar nao hawakua nyuma kuja muunga mkono Mwandosya kutangaza nia
  
 
Mstaafu Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila akiomba sala katika mkutano huo
  
Moja ya viongozi wa Dini ya kiislamu akiomba Dua katika mkutano huo
  
Kamanda mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mbeya, Yona Sonero akiwa na
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa wakimsikiliza kwa makini Mwandosya akitangaza nia
 
 
Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani waliokuja muunga mkono Mwandosya kwa kutangaza nia ya kugombea urais
 
 
 
 
 
Nianze kuwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,muweza wa yote kwa rehema nyingi alizotushushia kutuwezesha kuifikia siku hii ya leo.
Kwani hatukustahili zaidi ya wengi waliotutangulia mbele za haki.Nawashukuru ninyi nyote mliofika kuungana nami katika siku hii muhimu katika kukuza,kuimarisha na kuendeleza demokrasia ndani ya Chama chetu,Chama Cha Mapinduzi. 
Wazee wangu,  Waheshimiwa Maaskofu, Viongozi wa Dini na madhehebu mbalimbali,Waheshimiwa viongozi wa kimila,Waheshimiwa Machifu,akina mama,vijana,WanaCCM wenzangu,Viongozi wa vyama vya siasa,Wananchi,Wana Mbeya,Nawashukuru,Asanteni sana kwa uwepo wenu.
Ndugu zangu,
Kwa muda mrefu na kwa njia mbalimbali za mawasiliano mmekuwa mkinidadisi Mbona kimya kuhusu mwaka 2015? Pamoja nna kwambamliutaja mwaka tu, lakini niliwaelewa.
Wengi mliushangaa ukimya wangu.Pamoja na na kwamba ukimya ni sehemu ya haiba yangu na daima nimeupokea kama ni karama aliyonitunuku Mwenyezi Mungu,Muweza wa yote,baadhi yenu niliwajibu " Ukimya una Kishindo"! Kuhusu Sultan Qabus wa Oman,mwandishi mmoja maarufu aitwae Robert Kaplan amemwelezea ifuatavyo: Ni mtu mkimya, mpole, hapendi kuzungumza na waandishi wa habari mara kwa mara, hapendi habari zake ziandikwe kwenye magazeti mara kwa mara,lakini ameibadilisha nchi ya Oman kutoka makundi hasimu ya makabila na kuwa taifa linaloheshimika na linaloendelea kwa kasi sana na kuwa mfano wa kuigwa...." Sijifananishi na Sultan Qabus, la hasha.Isipokuwa najaribu kusisitiza kwamba mara nyingi ni bora katika maisha kuwa mjenga hoja na mtendaji makini kuliko kuwa  mpayukaji na maamuzi ya papo kwa papo yenye matokeo hasi na yenye hasara kwa taifa. Nimeenda nje kidogo ya mada yangu!
Kwa staili ya siku hizi wagombea watarajiwa huwa tunajitokeza na kusema : tutatangaza nia siku hii au ile! Nadhani tunawashangaza na mtuwie radhi.Kwani kwa kusema hivyo tunakua  tayari tumetangaza nia!Basi nami kwa staili hiyo hiyo naomba kutangaza rasmi mbele ya kadamnasi hii kama mashahidi,kwamba  kwa unyenyekevu mkubwa, nitaomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Natarajia kuendeleza rasmi safari niliyoianza leo kwa kuchukua fomu za maombi hayo pale Dodoma,Makao Makuu ya CCM, jumatano, tarehe 3 Juni,2015, saa 4 kamili,barabara.
Kipindi cha mpito kutoka awamu moja ya uongozi kwenda awamu nyingine kingekuwa kigumu sana kwa nchi nyingi hasa nchi zetu za kiafrika. Mifano iko wazi.Majirani zetu wamepata shida.Lakini waasisi wetu Hayati Mwalimu Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume wametujengea misingi imara.
 Tuna kila sababu ya kuwashukuru na tuna kila sababu ya kujivunia misingi hiyo. CCM haijayumba na CCM haitayumba.
Baadhi ya wanachama inawezekana wameyumba. Hebu tuzirudie Ahadi za mwana CCM: binadamu wote ni ndugu zangu na AFrika ni moja, nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote, nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma, rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa, cheo ni dhamana sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu binafsi, nitajielimisha kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote, nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu, nitakuwa mwanachama mwaminifu wa ccm na raia mwema wa Tanzania na Afrika nzima.
 Nitasema kweli daima fitna kwangu ni mwiko. Hii ndiyo CCM na atoaye ahadi mbele za Mwenyezi Mungu ndiye Mwana CCM,na si vinginevyo.
Ahadi ya mwanaCCM ya kuondoa umaskini inanipa nafasi ya kuelezea na kusisitiza kipaumbele muhimu sana cha serikali iliyodhamiria kuwaondoa wananchi wake kutoka lindi la umasikini ni kukuza uchumi,uchumi wa kisasa,uliojikita katika misingi ya sayansi na teknolojia na kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kama kichocheo cha maendeleo hayo.
 Kama sayansi na teknolojia  ndio msingi wa uchumi wa kisasa basi naweza kusema,tena kwa unyenyekevu mkubwa kwamba aliye mbele yenu ndiye pekee mwenye ujuzi,uelewa,na uzoefu wa masuala haya. Ninalotaka kusisitiza hapa ni kwamba kukuza na kusimamia uchumi ndio utakuwa kipaumbele namba moja.Jenga kwanza uchumi imara na mengine yatafuata.
 
Uchumi imara unajengwa hasa pale panapokuwa na lengo la kitaifa.Lengo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ni Tanzania kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. 
Lengo hilo liliwekwa mwaka 2000. Tudhamiria sasa kwamba ifikapo mwaka 2030 Tanzania iwe nchi  za juu zenye kipato cha kati(High Middle Income),na kwamba ifikapo 2050 Tanzania iwe nchi iliyoendelea.
Tunawezaje kuyafikia malengo hayo? Tunawezaje kukuza uchumi na ukuaji huo uwe endelevu?Hili ndilo swali.
1.Kilimo cha kisasa na cha kisayansi kupitia matumizi zaidi na bora ya mbolea; kuendeleza utafiti kwa kuboresha miundombinu,vifaa,na kuendekeza rasilimali watu;kuboresha mifumo na aina ya mikopo kwa wakulima wadogo;kuboresha barabara za vijijini; kuendeleza ujenzi wa maghala kwa ajili ya kutunza nafaka;kuwa na migumo ya uhakika ya masoko ya mazao;na kuhakikisha kiwanda cha kimkakati cha mbolea itokanayo na gesi asilia kinajengwa haraka iwezekanavyo.
2.Kuanzisha na kuendeleza viwanda,kwa kuanzia viwanda vinavyoongeza thamani ya mazao na rasilimali asili
3.Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula.
4.Kuendelea kusimamia kutengemaa kwa uchumi mpana
5.Kuondoa vikwazo vinavyozuia uwekezaji wa ndani na kutoka nje
6.Kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa ipasavyo kwa kufungua fursa nyingi za utalii wa ndani na utalii katika sekta ya kusini.
7.Kuongeza tija katika utendaji wa kazi kwa kuthamini kazi(kufanya kazi kwa bidii,kwa uadilifu,na kwa kujituma), kusimamia kanuni,maadili na miiko ya utumishi wa umma na kuufanya utumishi wa umma usiwe wa mazoea tu bali wa ushindani unaopimika katika kutoa huduma kwa wananchi.Hii itakwenda sambamba na kulinda haki na kuboresha msilahi ya wafanyakazi.
8.Kuchukia,kuzuia na kupambana na ufisadi na rushwa. Kuondoa vikwazo vinavyoonekana kuwepo  kwa matabaka mawili ya wananchi; wale wanaoshughulikiwa na takukuru moja kwa moja,na wale ambao kibali kinahitajika kuwashtaki,kwa kuipa Takukuru uwezo wa kisheria kufanya kazi bila kuingiliwa na chombo chochote,wakati huohuo kuhakikisha haki za wananchi wema zinalindwa kupitia chombo cha kusimamia malalamiko (ombudsman).
9.Kuendeleza na ikibidi kuimarisha uhuru wa Benki Kuu  na uhuru wa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi,mifuko ya jamii,bima.
10.Serikali kuwa injini ya ukuaji wa uchumi lakini kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi,mtu mmoja,vikundi vya wajasiriamali,saccos,na kampuni binafsi kuchochea ukuaji wa uchumi.
 Uchumi unapokua,basi serikali itakuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza vipaumbele katika maendeleo ya jamii: Elimu,maji safi na salama,afya, na miundombinu.
 Kuhusu elimu,lengo litakuwa ni kuboresha mitaala ili iendane na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ngazi zote;kuhakikisha kila mtanzania ana nafasi sawa ya kujiendeleza kielimu kuanzia ngazi ya awali mpaka elimu ya juu; kuendeleza elimu ya ufundi na kilimo; kuandaa na kutekeleza mipango kwa hatua kuifanya elimu ya msingi ifikie kidato cha pili, cha nne na hatimaye kidato cha sita;kuongeza wingi wa udahili  wa wasichana katika katika ngazi ya elimu ya juu;kuboresha hali na ari ya utendaji wa  kazi kwa walimu,ikiwa ni pamoja na ujenzi nyumba za kuishi na kuongeza ujira.
Katika maeneo mengine ya huduma za kijamii,lengo la serikali litakuwa ni kutekeleza sera zilizopo na kuhakikisha malengo yanatekelezwa na yanapimika.Katika kuleta afya bora kwa wananchi lengo litakuwa ni kuweka mizania katika kuzuia na kupambana na magonjwa.
Uchumi hauwezi kukua pasipokuwa na amani na utulivu. Amani usalama na utulivu ni tunu.Waasisi wetu wametujengea msingi wa tunu hii. 
Viashiria vya kupotea kwa amani vinaanza kuonekana kutoka ndani na nje.Hali inahitaji kuimarisha vyombo vyetu vya usalama katika maeneo yote hususan mafunzo,vitendea kazi,vifaa, miundombinu na silaha za kisasa.Hatimaye ulinzi wa nchi unaanzia mwananchi mwenyewe.
Nafasi ya Zanzibar katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni kubwa. Hii inatokana na asili na haiba ya nchi zenye visiwa,Zanzibar ikiwa mojawapo. Historia ya Zanzibar inatukumbusha hili.Kwani katika karne ya kumi na tisa Zanzibar iliongoza eneo lote la Afrika ya Mashariki kiuchumi na maendeleo,ukuondoa biashara ya utumwa. 
Ilisemekana Ikipigwa zumari Zanzibar wanacheza ngoma maziwa makuu. Kila linalowezekana litafanywa kuondoa kabisa hali inayoweza kuikwaza Zanzibar kufikia uwezo wake mkubwa kiuchumi.Muungano utaimarika na uchumi wa Tanzania utakuwa kwa kasi zaidi.
Nahitimisha na suala muhimu la uzalendo.Kwa tafsiri isiyo rasmi,Uzalendo  ni upendo kwa nchi. Tumeanza kushuhudia kupungua kwa uzalendo. Upungufu huo unajionesha katika kuenzi tamaduni za nje,kubeza juhudi za maendeleo yaliyopatikana, viongozi kutoa matamshi yanayo kebehi nchi wakiwa nje ya nchi,kutojivunia historia yetu iliyojikita katika michango ya mashujaa wetu. 
Hawa ni pamoja na  wale waliopambana na wakoloni,akina Kinjeketile,  Mkwawa ,Mirambo,Chaburuma na wengineo ambao walitoa uhai wao kulinda na kutetea heshima ya mwafrika dhidi ya ukoloni.Aidha waasisi wa TANU,Hayati Mwalimu Nyerere,Sykes,Mzee Kawawa, na wenzao;Waasisi wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Hayati Abeid Amani Karume na wenzake akina Mzee Thabit Kombo,Kanali Seif Bakari,Hais Darwesh,Edington Kisasi,Yusuf Himid,Said Washoto na wengineo;ambao walionesha upendo na uzalendo wa hali ya juu.Vilevile tuna mashujaa wa ukombozi wa Kusini mwa Afrika akina George Magombe na Hashim Mbita.Tutaendelea kuenzi, kuthamini,na kuiendeleza  michango mikubwa ya Marais wetu wastaafu,Mzee Aboud Jumbe, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Hayati Idris Abdukwakil,Dr Salmin Amour,Dr Amani Abeid Karume,na Mzee Benjamin William Mkapa. Kipekee napenda kuwashukuru Marais wetu wa sasa; Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mheshimiwa Dr Ali Mohamed Shein.ambao wamefanya kazi kubwa ya kuimarisha uchumi na umoja wa nchi yetu. Daima nitaenzi mchango wao. Tujivunie nchi yetu na  Kwa pamoja tutaenga nchi tunayoitaka.
 
 

Monday, June 1, 2015

ZIJUE FAIDA ZA KULA MATUNDA


Kuna faida nyingi za kujenga mwili wako zinazotokana kwa kula matunda. Licha ya kupenda ladha tamu za matunda mbalimbali,  matunda yana virutubisho vingi kama vitamin na madini. Vitamin A na C hupatikana kwenye matunda mengi ukilinganisha na virutubisho vingine vilivyopo kwenye matunda ya aina mbalimbali.

Matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo( heart diseases ), stroke (kiharusi ), shinikizo la damu ( blood pressure ), cholesterol, aina mbalimbali za saratani (cancer ), matatizo ya uwezo wa macho kuona na mengine mengi.


Matunda yote yana manufaa mwilini kwa afya lakini napenda ujue faida kadhaa zinazopatikana kwenye apple, parachichi, ndizi, zabibu, embe, chungwa, papai na nanasi.



Zijue faida mbalimbali zitokanazo kwa kula matunda yafuatayo

1. APPLE

 

 
Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari ( diabetes ) na pumu (asthma )
Husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya ( natural mouth fresher ) vilevile apple husafisha meno unapotafuna.





Harufu nzuri ya apple hupatikana kwenye maganda/ngozi yake, hivyo ni vyema ukalitafuna pasipo kulimenya kwani vitamin nyingi pia hupatikana kwenye maganda/ngozi ya juu ya apple. 


2. PARACHICHI
 
  • Ni chanzo cha vitamin E.
  • Hupunguza kiwango cha cholesterol mwilini kwakuwa halina mafuta mengi sana ukilinganisha na nyama au mbegu zitoazo mafuta.
Kwa afya njema ya moyo wako, kwenye sandwich au mkate tumia parachichi badala ya siagi.
  
Watoto hupenda sana kula parachichi kwasababu ni laini na pia mafuta ya parachichi husaidia katika kukuwa vizuri kwa mtoto na kuwa mwenye afya bora.


3. NDIZI
 
  • Ni chanzo cha vitamin B6 na madini ya potassium.
  • Licha ya kuwa na ladha nzuri, ndizi zina madini mengi ya potassium ukilinganisha na matunda mengine ambayo husaidia kupunguza ongezeko la shinikizo la damu ( blood pressure ).
Watu wenye aleji na material ya mpira( rubber latex ) wanaweza pia kuathirika kwa aleji ya ndizi kwakuwa mpira na ndizi vyote zina aina moja ya protini.

4. ZABIBU
  • Ni chanzo cha madini ya manganese.
  • Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa kusaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu ( blood pressure )
  • Huepusha magonjwa ya aina mbalimbali za saratani kwa kuzuia usambaaji wa seli za saratani ya titi ( breast cancer ), tumbo ( stomach cancer ) na utumbo ( colon cancer ).
Unaweza gandisha zabibu za kijani na nyekundu na ukazitumia kama barafu ( ice cubes ) kwenye kinywaji chako upendacho.


5. EMBE
 

  • Ni chanzo cha vitamin A na E.
  • Vitamin A  iliyopo kwenye embe husaidia kuboresha macho yako kwa kukuwezesha uweze kuona vizuri. Pia husaidia kupunguza uwezekano wa kupata upofu kwa wazee kwa kuimarisha macho.
Embe ni tamu sana likiwa limeiva lakini pia likiwa bichi unaweza kutumia embe kutengenezea kachumbari, achali, chutney na salad.

6. CHUNGWA


  • Ni chanzo cha vitamin C na madini ya potassium.
  • Chungwa lina vitamin inayojulikana kama ‘’folate’’ ( B-Group Vitamin ) ambayo husaidia katika kujengeka kwa ubongo wa mtoto kwa mama mjamzito.
  • Chungwa lina kemikali zinazojulikana kama ‘’hesperidin’’ ambazo hupunguza kiwango cha cholesterol kwenye damu.
Sehemu nyeupe ya chungwa ( gome lililo ndani ya chungwa ) lina thamani ya vitamin karibia sawa na nyama ya chungwa hivyo ni vyema kula chungwa lote baada ya kumenya maganda yake.
 7. PAPAI

  • Ni chanzo cha vitamin A na C.
  • Papai lina enzyme ijulikanayo kama ‘’papain’’ ambayo husaidia katika usagaji au mmeng’enyeko wa chakula.
  • Pia vitamin A iliyopo kwanye papai husaidia husaidia kuboresha afya ya ngozi yako.
Mbegu nyeusi za papai zinaweza kuliwa japo kuwa ni chungu lakini unaweza kuzisaga na salad kwa kutumia blender na zina faida sawa na kula pilipili.


 8. NANASI

  • Nanasi lina enzyme asilia ijulikanayo kama ‘’bromelain’’ ambayo husaidia kuvunjavunja  protini hivyo husaidia katika mmeng’enyeko au usagaji wa chakula.
  • Vilevile enzyme ya bromelain husaidia kupunguza ukuaji wa seli za saratani na kuchochea uponaji wa vidonda kwa haraka.
Kwa hayo machache hapo juu unaona ni jinsi gani matunda yalivyo muhimu kwa kujenga afya zetu ambapo matunda yanaweza kutumika kama dawa kwa miili yetu. Napendekeza upende kula angalau tunda moja kwa siku kwa uboreshaji na uimarishaji wa afya yako. 

FAIDA 17 ZA MAZOEZI MWILINI MWAKO


Mazoezi ni muhimu kwa afya, kuna mazoezi ya aina mbalimbali. Unaweza kufanya mazoezi ya viungo au sehemu ya mwili kama tumbo, miguu, mikono, mgongo n.k. Vilevile kuna mazoezi ya kuchangamsha na kupasha mwili mfano mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba na mengineyo. 

Licha ya kuwa unaweza kutumia muda kidogo kufanya mazoezi kwa takribani dakika (30-45) kwa siku iwe asubuhi au jioni, mazoezi yana faida nyingi kiafya. Kama ifuatavyo..!!

1. Mazoezi hukufanya uchangamke na kuwa shupavu.

2. Mazoezi huboresha ufahamu wako, uwezo wa kuelewa na kufikiri mambo katika mazingira yanayokuzunguka.

3. Mazoezi huboresha uwezo wa ubongo kuhifadhi kumbukumbu.

4. Mazoezi hupunguza msongo wa mawazo.

5. Mazoezi huimarisha moyo hivyo huepusha maradhi yatokanayo na mapigo mabaya ya moyo.

6. Mazoezi humfanya mtu ajiamini kwa kupunguza stress, tension, wasiwasi n.k

7. Mazoezi hupasha mwili joto hivyo husaidia kuzuia na kupunguza baridi.

8. Mazoezi husaidia kuweka sawa kiwango cha cholesterol na mafuta yaliyopo mwilini.

9. Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa kisukari.

10. Mazoezi hushusha kupanda kwa shinikizo la damu.

11. Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata baadhi ya maradhi ya saratani.

12. Mazoezi humsaidia mtu kuondokana na baadhi ya matatizo ya akili.

13. Mazoezi huongeza hamu ya mtu kutaka kula.

14. Mazoezi hupunguza uzito wa ziada wa mwili na kufanya mwili wako kuwa mwepesi.

15. Mazoezi huimarisha mifupa hivyo hupunguza matatizo yatokanayo na kudhohofika kwa mifupa jina la kitaalamu.

16. Mazoezi huboresha kinga ya mwili.

17. Mazoezi husaidia kuweka sawasawa mifumo mbalimbali ya mwili. Mfano: mfumo wa ufahamu, mzunguko wa damu, homoni na misuli.

Hizi ni baadhi ya faida za kufanya mazoezi, yote ya yote mazoezi hurefusha maisha kwa kukufanya uwe mwenye afya njema. Ni vyema ukajiuliza, hivi ni kweli kufanya mazoezi na kula vizuri (vyakula bora) ni kuboresha maisha yako? Jibu ni NDIYO mazoezi na vyakula ni dawa pekee ya kutibu au kukuepusha na magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika. Fanya mazoezi kuimarisha afya yako!

WANASAYANSI WATENGENEZA MBEGU ZA KIUME KWA AJILI YA WANAUME WASIO NA UWEZO WA KUPATA WATOTO


Seli za mbegu za kiume zimetengezwa katika maabara kwa mara ya kwanza na hivyo basi kuwapa matumaini wanaume wasio na uwezo wa kupata watoto.

Kampuni moja nchini Ufaransa imedai kwamba imefanikiwa kubadilisha vipande tofauti vya maumbile hadi kupata mbegu za kiume zinazoweza kutoa mtoto kwa mara ya kwanza.

Iwapo uzinduzi huo utathibitishwa ,huenda ukabadilisha maisha ya wanaume wengi duniani ambao hawawezi kutoa mbegu za kiume.

Maabara ya Kallistem,kituo cha kibinafsi cha utafiti kilichopo mjini Lyon kimesema kuwa kitaweza kufanya majaribio katika kipindi cha miaka miwili.
Iwapo uzinduzi huo utaingia sokoni,kampuni hiyo inataraji kuwatibu watu 50,000 kila mwaka soko ambalo linaweza kuwa na thamani ya pauni bilioni 1.7 .

Hatahivyo matokeo ya utafiti huo hayajachapishwa ama hata kuthibitishwa huku wataalam wa Uingereza wakichukulia uvumbuzi huo kama uvumi tu.

Kalliste imesema kuwa imefanikiwa kubadilisha seli za kawaida katika mbegu za kiume hadi mbegu za kiume zilizokomaa.