Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo
kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe
umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia.
Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii
Kwenye
treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni
mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa
kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za
macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.
Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa
huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na
isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa
wanawake.
Rafiki yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu
kwenye kidevu kila kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa
upasuaji wa pua na akashawishiwa -ama akajishawishi- kuwa ni mikunjo ya
kidevu chake iliyohitaji kubadilishwa.
Matokeo,kidevu chenye umbo
bora zaidi lakini chenye uchungu zaidi.Licha ya hayo,anadhamiria
kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.
Kilio cha uchungu baada ya upasuaji wa pua ili kunyooshwa.
Katika nchi hii,wazazi wananielezea kuwa wanawapa mabinti zao zawadi
ya 'upasuaji maradufu wa vibugiko vya macho'' inayowezesha macho yao
kuonekana zaidi-''kwa kweli huku ni kupunguza maumbile ya Kiaasia.Sijui
mbona kwani macho ya Kikorea yanavutia sana vile yalivyo.
''Msisitizo
unaotolewa na matangazo ya aina hii kwenye treni ni kuwa ''kujiamini
jinsi unayoonekana hukupa nguvu ambayo yaweza kuwa chanzo cha
furaha.''Furaha ambayo inayopatikana kwa kukatwa kwa kisu!!!
Isipokuwa
kwamba si hivyo.sasa kuna kesi kadhaa kotini ambapo wagonjwa-ama
waathirika kama wanavyojulikana- wanawashitaki madaktari waliopangua na
kupanga tena nyuso zao,kwa njia wasizopenda wao.Muathiriwa mmja alisema
''hii si sura ya binadamu'' punde alipovua bandeji.
Hii si sura ya binadamu,ni maasi kuliko wa hayawani ama majitu.''
Baada ya upasuaji wa kuongeza ukubwa wa matiti, mwanamke huyu badala yake akapatwa na kasoro ya titi moja kubwa na lengine dogo.
Kim Bok-soon alitumia Won milioni 30 (£17,320) kwa jumla ya upasuaji
mara 15 kwenye uso wake katika kipindi cha siku moja na baadaye
akagundua kuwa daktari wake hakuwa mpasuaji wa kuongeza urembo bandia
mwilini ambaye alimhadaa Kim BoK-Soon kutumia won (17,320) kufanya
upasuaji mara 15 kwenye uso wake.
Sehemu ya shida ni kuwa upasuaji
wa kuongeza urembo bandia una faida kubwa na kwa hivyo unawaalika
madaktari wengi ambao hawajahitimu- ama madaktari wale waliohitimu
katika nyanya zingine za utabibu.
Inadaiwa kuwa taratibu
zimefanywa na wanaoitwa ''madaktari mapepo''.Katika kesi moja
kotini,inadaiwa kuwa daktari alihepa chumba cha upasuaji wakati mgonjwa
wake akiwa kwenye dawa za kuondoa fahamu na kupunguza uchungu na kuwacha
kazi hiyo kufanywa na mpasuaji mwingine badala yake.
Juu ya hiyo,
iliibuka kuwa madakatari hao wamejifanyia upasuaji wa kujiongeza urembo
bandia kuilingana na picha zao kabla - na - baada ya upasuaji.
Kwa
uhakika ni kwamba Chama cha madaktari wa upasuaji wa kuongeza urembo
bandia Korea kimetoa wito kwa kuwepo na sheria kali ya madaktari na
wanaotoa ujumbe. Wanahofia kwamba utangazaji mbaya unaharibu sifa ya
sekta ambayo kwa kiasi kikubwa imesimamiwa vizuri.
Sio China peke yake ambko biashara ya urembo bandia imenoga hata Venezuela ambako wanawake wanapenda sana makalio bandi.
Lakini wao wanapigana na mseto huu, Upasuaji una faida sana, hata una
bei ambazo zinadhoofisha upasuaji huo Marekani na Ulaya. Ni biashara
kubwa sana huko Gangnam, hapa katika Seoul, bei ya "kurekebisha jicho"
ni dola 1500 na ni shughuli inayochukua dakka 30 tu. hiyo huongezeka
hadi dola 11,000 kwa upasuaji wa kurekebisha sura.
Lakini labda
watu wa China ambao wanataka kuwa kwenye filamu au, wazazi wa Korea
Kusini ambao wanadhani wanaweza kuwarembesha mabinti wao kupitia kisu
cha upasuaji lazima watafakari njia ya kushtua ya kupitia kwenye
mahakama.
Malkia aliyekuwa mshindi wa taji la urembo, alifanyiwa
upasuaji wa kukuza kifua ambayo ilikuwa na madhara makubwa mno kwani
upasuaji huo ulifanya titi lake moja kuwa kubwa kuliko lingine.
Analaumu
madaktari kwa kushindwa na matibabu na pia kwa kutomweleza kwa uwazi ".
Angalia, huna haja ya upasuaji huu" "Upasuaji wa plastiki ni kama
madawa ya kulevya," alisema. "Kukishafanya macho, utataka pua."
Na
madaktari pia hawakwambii kuwa "uko mrembo sana ulivyo bila upasuaji"
Masaibu yanayokupata baadaye kutokana na madhara ya upasuaji huo huwa ni
juu yako mwenyewe.
No comments:
Post a Comment