Thursday, December 18, 2014

TATIZO LA WAMACHINGA NA OMBA OMBA MAENEO YASIYORUHUSIWA DAR KUTAFUTIWA DAWA

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akifuangua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) leo jijini Dar es salaam.


Jiji la Dar es salaam linaangalia upya utaratibu wa kuwaondoa ombaomba na wafanyabiashara ndogondogo(wamachinga)  katika maeneo yasiyoruhusiwa katika jiji la Dar es salaam kufuatia sheria na hatua zinazochukuliwa ikiwemo kuwarudisha ombaomba hao katika mikoa wanayotoka kutokuzaa matunda na kuwa endelevu kufuatia wengi wao kurudi katika maeneo ya awali kila wanapoondolewa.
 
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki wakati akifungua kikao cha wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) kilichofanyika leo jijini Dar es salaam kujadili masuala mbalimbali ya mendeleo katika jiji la Dar es salaam.
 
Amesema kuwa kuendelea  kuwepo kwa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi ni moja ya changamoto inayolikabili jiji la Dar es salaam kutokana na biashara wanazozifanya kuchangia kuzuia maeneo ya barabara ya waenda kwa miguu, kusababisha uchafuzi wa mazingira,kusabisha msongamano wa magari kwa baadhi yao kuweka bidhaa  barabarani.
 
Amesema kutokana na hali hiyo baadhi ya wafanyabiashara walio na biashara rasmi  ambao hulipa kodi za Serikali wamekuwa wakilamikia hali  ya ukwepaji wa kodi inayofanywa na wafanyabiashara hao.
 
Bw. Sadiki amesema mpango wa mkoa wa sasa ni kuendelea kuwatumia wafanyabiashara hao kama  fursa ya mtaji wa rasilimali watu ambayo itatumika kama chanzo cha mapato katika kuleta maendeleo ya mkoa.
 
Amesema watendaji na viongozi wa halmashauri za mkoa wa Dar es salaam wanalojukumu la kuweka mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao na kuwatumia katika shughuli za uzalishaji kwa utaratibu mzuri utakaowekwa ili waendelee kunufaika na shughuli wanazofanya. 
Akizungumzia kuhusu uboreshaji wa huduma za jamii zikiwemo za Maji, Elimu na Afya katika jiji la Dar es salaam  amesema kuwa Serikali inaendelea kuzijengea uwezo shule kwa kuongeza majengo ya madarasa, maabara na kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaofaulu elimu ya msingi wanapata fursa ya kuendelea na masomo ya Sekondari.
 
Kuhusu huduma za afya amesema kuwa mkoa unaendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo la ghorofa nane, eneo la Magomeni katika manispaa ya Ilala litakalotumika kutolea huduma ya Afya ya Mama na Mtoto na kuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 500.
 
“  Sasa tuko kwenye maandalizi ya ujenzi wa jengo maalum la kutolea huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika jiji la Dar es salaam litakalogharimu zaidi ya shilingi bilioni ishirini na moja, tayari benki ya Tanzania Investment Bank imeshakubali kutoa mkopo kwa ajili ya jengo hilo” Amesisitiza.
 
Aidha, katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametoa ufafanuzi kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchi nzima  Desemba 14 mwaka huu na kueleza kuwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam ambayo uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vurugu, uchaguzi huo utarudiwa ndani ya siku saba.
 
Ameeleza kuwa katika mkoa wa Dar es salaam uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika kwenye mitaa 561 lakini kutokana na changamoto mbalimbali ulifanyika kwenye mitaa 491 na kuahirishwa kwenye kata 70.
 
Amelitaka jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa linaimarisha ulinzi na usalama wakati wa marudio ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika ndani ya siku 7 katika mitaa yote ambayo uchaguzi uliahirishwa .

Wednesday, December 17, 2014

Roboti zapata ajira mgahawani China





















Roboti ikimuhudumia mteja 

Mgahawa mmoja nchini China umeanza kutumia Roboti badala ya kuwaajiri wafanyakazi wa hotelini kuwapakulia chakula na vinywaji wageni. Hebu tazama mambo yalivyo

bbc.com

TAHADHARI:'Hatari za urembo bandia'

Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia.

Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii

Kwenye treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.


Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake.

Rafiki yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu kwenye kidevu kila kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa upasuaji wa pua na akashawishiwa -ama akajishawishi- kuwa ni mikunjo ya kidevu chake iliyohitaji kubadilishwa.

Matokeo,kidevu chenye umbo bora zaidi lakini chenye uchungu zaidi.Licha ya hayo,anadhamiria kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.

Kilio cha uchungu baada ya upasuaji wa pua ili kunyooshwa.


Katika nchi hii,wazazi wananielezea kuwa wanawapa mabinti zao zawadi ya 'upasuaji maradufu wa vibugiko vya macho'' inayowezesha macho yao kuonekana zaidi-''kwa kweli huku ni kupunguza maumbile ya Kiaasia.Sijui mbona kwani macho ya Kikorea yanavutia sana vile yalivyo.

''Msisitizo unaotolewa na matangazo ya aina hii kwenye treni ni kuwa ''kujiamini jinsi unayoonekana hukupa nguvu ambayo yaweza kuwa chanzo cha furaha.''Furaha ambayo inayopatikana kwa kukatwa kwa kisu!!!

Isipokuwa kwamba si hivyo.sasa kuna kesi kadhaa kotini ambapo wagonjwa-ama waathirika kama wanavyojulikana- wanawashitaki madaktari waliopangua na kupanga tena nyuso zao,kwa njia wasizopenda wao.Muathiriwa mmja alisema ''hii si sura ya binadamu'' punde alipovua bandeji.

Hii si sura ya binadamu,ni maasi kuliko wa hayawani ama majitu.''

 

 Baada ya upasuaji wa kuongeza ukubwa wa matiti, mwanamke huyu badala yake akapatwa na kasoro ya titi moja kubwa na lengine dogo.


Kim Bok-soon alitumia Won milioni 30 (£17,320) kwa jumla ya upasuaji mara 15 kwenye uso wake katika kipindi cha siku moja na baadaye akagundua kuwa daktari wake hakuwa mpasuaji wa kuongeza urembo bandia mwilini ambaye alimhadaa Kim BoK-Soon kutumia won (17,320) kufanya upasuaji mara 15 kwenye uso wake.

Sehemu ya shida ni kuwa upasuaji wa kuongeza urembo bandia una faida kubwa na kwa hivyo unawaalika madaktari wengi ambao hawajahitimu- ama madaktari wale waliohitimu katika nyanya zingine za utabibu.

Inadaiwa kuwa taratibu zimefanywa na wanaoitwa ''madaktari mapepo''.Katika kesi moja kotini,inadaiwa kuwa daktari alihepa chumba cha upasuaji wakati mgonjwa wake akiwa kwenye dawa za kuondoa fahamu na kupunguza uchungu na kuwacha kazi hiyo kufanywa na mpasuaji mwingine badala yake.

Juu ya hiyo, iliibuka kuwa madakatari hao wamejifanyia upasuaji wa kujiongeza urembo bandia kuilingana na picha zao kabla - na - baada ya upasuaji.

Kwa uhakika ni kwamba Chama cha madaktari wa upasuaji wa kuongeza urembo bandia Korea kimetoa wito kwa kuwepo na sheria kali ya madaktari na wanaotoa ujumbe. Wanahofia kwamba utangazaji mbaya unaharibu sifa ya sekta ambayo kwa kiasi kikubwa imesimamiwa vizuri.


 Sio China peke yake ambko biashara ya urembo bandia imenoga hata Venezuela ambako wanawake wanapenda sana makalio bandi.


Lakini wao wanapigana na mseto huu, Upasuaji una faida sana, hata una bei ambazo zinadhoofisha upasuaji huo Marekani na Ulaya. Ni biashara kubwa sana huko Gangnam, hapa katika Seoul, bei ya "kurekebisha jicho" ni dola 1500 na ni shughuli inayochukua dakka 30 tu. hiyo huongezeka hadi dola 11,000 kwa upasuaji wa kurekebisha sura.

Lakini labda watu wa China ambao wanataka kuwa kwenye filamu au, wazazi wa Korea Kusini ambao wanadhani wanaweza kuwarembesha mabinti wao kupitia kisu cha upasuaji lazima watafakari njia ya kushtua ya kupitia kwenye mahakama.

Malkia aliyekuwa mshindi wa taji la urembo, alifanyiwa upasuaji wa kukuza kifua ambayo ilikuwa na madhara makubwa mno kwani upasuaji huo ulifanya titi lake moja kuwa kubwa kuliko lingine.

Analaumu madaktari kwa kushindwa na matibabu na pia kwa kutomweleza kwa uwazi ". Angalia, huna haja ya upasuaji huu" "Upasuaji wa plastiki ni kama madawa ya kulevya," alisema. "Kukishafanya macho, utataka pua."

Na madaktari pia hawakwambii kuwa "uko mrembo sana ulivyo bila upasuaji" Masaibu yanayokupata baadaye kutokana na madhara ya upasuaji huo huwa ni juu yako mwenyewe.


chanzo ni BBCSwahil


Sunday, November 9, 2014

UWATA BOYS HIGHT SCHOOL

Jengo la Madarasa ya Uwata boys school
Jengo la utawala
Hostel
Ukumbi
Kwa maelezo zaidi tembelea Hapa

Friday, November 7, 2014

AJALI YATOKEA VWAWA MBOZI LEO MCHANA

Habari zaidi tembelea www.mkwinda.blogspot.com

WANUSURIKA KIFO BAADA YA BASI LA HAPPY NATION KUPINDUKA IGURUSI MBEYA

Majeruhi wakiwa hospitali ya chimala

 Majeruhi wakisubiri usafiri waende hospitali chimala Mbeya

Ajari hii imetokea leo asubuhi maeneo ya Igurusi kwa habari kamili tembelea

Mbeya yetu

HAKI YA MTUHUMIWA MBELE YA POLISI




1. Mtuhumiwa ni nani?
Ni mtu yeyote ambaye anawekwa chini ya ulinzi na
polisi au chombo cha usalama kwa kutuhumiwa
kufanya kosa la jinai.
2. Makosa ya jinai ni yapi?
Ni makosa ambayo mtu akipatikana na hatia hupe-
wa adhabu.
Ni makosa kama wizi, ubakaji, mauaji, kufanya
makosa ya kuhatarisha amani n.k.
3. Haki za Mtuhumiwa
(a) Mtuhumiwa anapowekwa chini ya ulinzi
ana haki ya kuelezwa sababu za kukamatwa
au kutiliwa mashaka.
(b) Mtuhumiwa ana haki ya kudai risiti ya orodha
ya vyombo/mali atakayokuwa nayo wakati
wa kumpekua zile zinazochukuliwa kituoni na
pale anapokabidhiwa polisi.
(c) Mtuhumiwa akiwa mwanamke lazima
kukaguliwa na polisi mwanamke.
(d) Mtuhumiwa ana haki ya kudai kibali cha
hakimu pale majadiliano/maelezo kwa polisi
yanapozidi saa nane.
(e) Mtuhumiwa anayo haki ya kudai awasiliane na
mtu anayemtaka akiwa chini ya ulinzi.
Kwa mfano rafiki, ndugu au wakili.
(f) Mtuhumiwa ana haki ya kufikishwa
mahakamani katika muda usiozidi masaa 24.
(g) Mtuhumiwa ana haki ya kukaa kimya wakati
wa mahojiano na polisi na anapaswa kuelezwa
kwamba chochote ambacho mtuhumiwa
atawaeleza polisi inaweza kutolewa
mahakamani kama ushahidi dhidi yake.
(h) Mtuhumiwa ana haki ya kutojibu maswali
ya polisi na kukaa kimya hadi polisi
anayemuuliza/endesha mahojiano awe
amemueleza mtuhumiwa yafuatayo:
(i) cheo alicho nacho na jina lake
(ii) mtahadharishwa kwamba yuko chini ya ulinzi.
(iii) kosa alilofanya au sababu ya kuwa chini ya ulinzi.
(iv) anayo haki ya kudai asomewe kilichoandikwa
kabla ya kuweka sahihi kwenye maelezo.
Mtuhumiwa anayo haki ya kupewa heshima na
kuthaminiwa kwamba ni binadamu. Hakuna ruhusa
kumtesa mtuhumiwa na kumdhalilisha anayo haki
ya kudai matibabu.
(i) Mtuhumiwa anaweza akaomba dhamana wakati
yuko chini ya ulinzi wa polisi.