Friday, March 27, 2015

ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO



Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi. "Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali kaldinari Pengo soma Zaidi

RUBANI WA NDEGE YA UJERUMANI ILIYOPATA AJALI NCHINI UFARANSA ALIANGUSHA KIMAKUSUDI


Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.
 
Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.Bwana Robin alisema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.
 
 
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliyokuwa inatoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwaua abiria wote 144 pamoja na wafanyakazi sita wa ndege.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vile vile tunasikia sauti ya kiti kikisonga nyumana mlio wa mlango ukifungwa," Bwana Robin aliwaambia waandishi wa habari.

MAGAZETI LEO 27 MARCH 2015


























Ajali ya Treni na Lori kati ya Machinga Complex na Mataa ya Chang'ombe



Ajari ya Treni na Lori imetokea machinga complex na mataa ya chang'ombe
wanaotumia njia hii tumien nyingine maana hapapitiki.

Saturday, March 14, 2015

TAZAMA PICHA 5 ZA JUMBA LA KIFAHARI ANALOISHA SPIKA WA BUNGE DODOMA


Hatimaye Spika wa Bunge la Tanzania pale Dodoma atakuwa na makazi rasmi baada ya ujenzi wa nyumba ya Spika kukamilika na makabidhiano kufanyika.
Nyumba hiyo ambayo ipo maeneo ya Uzunguni nje kidogo ya Dodoma mjini imegharimu takribani Tshs 1.5  Billion na imejengwa na kampuni ya Pacha Building Construction Company.  Hii inakuwa nyumba ya kwanza rasmi ya Spika kwani hapo awali hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya Spika.




Picture
Mlango wa mbele
Picture 
Upande wa nyuma wa jengo

Picture
Ngazi ndani ya jengo ambalo lina vyumba vinne vya kulala, sehemu ya mapumziko, sehemu ya chakula, maktaba na jiko.
chanzo The Choice

Monday, March 2, 2015

Rais Kikwete aongoza maelfu ya waombolezaji kuaga mwili wa Kapteni John Komba







Jeneza lenye mwili wa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,Marehemu Kapteni John Komba likiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam,wakati wa shughuli ya kuaga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI NA EMMANUEL MASSAKA.
 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
 
 Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
 
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
 
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
 
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo 
 
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiifariji familia ya marehemu. 
 
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,Luteni Kanali Samuel Ndomba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
 
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho akifuatana na Naibu IGP,Abdulrahman Kaniki. 
 
Kingunge Ngombale–Mwiru akitoa heshima za mwisho. 
 
Kamanda Kova. 
 
Baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wakiifariji familia ya Marehemu. 
 
Mhe. Ole Sendeka akibubujikwa na machozi kuondokewa na Mbunge mwenzake. 
 
Familia ya Marehemu. 
 
 Read More